Ugonjwa wa mtoto mchanga kufa ghafla
Ugonjwa wa mtoto mchanga kufa ghafla | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Magonjwa ya watoto |
Dalili | Kifo cha mtoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja[1] |
Muda wa kawaida wa kuanza kwake | Hutokea kwa ghafla[1] |
Visababishi | Hakijulikani[1] |
Sababu za hatari | Kulala kifudifudi (kulalia tumbo) au upande, joto kupita kiasi , kufiduliwa kwa moshi wa tumbaku, kutumia kitanda kimoja[2][3] |
Njia ya kuitambua hali hii | Hakuna sababu iliyopatikana baada ya uchunguzi na uchunguzi wa maiti[4] |
Utambuzi tofauti | Maambukizo, matatizo ya kijeni, matatizo ya moyo, unyanyasaji wa watoto[2] |
Kinga | Kuwalaza chali (kwa mgongo) watoto wachanga, kutumia titibandia, unyonyeshaji wa mtoto, utoaji chanjo[5][6][7] |
Matibabu | Kutoa huduma za kuwaliwaza familia zilizoathirika[2] |
Idadi ya utokeaji wake | mtu 1 kati ya watu 1,000–10,000[2] |
Ugonjwa wa mtoto mchanga kufa ghafla (kwa Kiingereza: Sudden infant death syndrome, kifupi: SIDS; unajulikana pia kama cot death au crib death) ni kifo cha ghafla cha mtoto wa chini ya mwaka mmoja ambacho chanzo chake hakijulikani.[1] Utambuzi wake unahitaji kwamba chanzo cha kifo hicho kisalie kama hakijulikani hata baada ya uchunguzi wa kina wa maiti na uchunguzi wa kina wa eneo la kifo kufanywa.[4] SIDS kwa kawaida hutokea mtoto akiwa amelala.[2] Kwa kawaida, kifo hutokea kati ya saa 00:00 na 09:00 [8] na kwa kawaida hakuna ushahidi wa kelele au wa kupambana.[9]
Kisababishi halisi hakijulikani.[3] Mahitaji ya mchanganyiko wa mambo yanayojumuisha uwezekano mahususi wa kuathiriwa, wakati mahususi katika kukua, na kishinikizo cha kimazingira yamependekezwa.[2][3] Vishinikizo hivi vya kimazingira vinaweza kujumuisha kulala kifudifudi (kulalia tumbo) au upande, joto kupita kiasi na kufiduliwa kwa moshi wa tumbaku.[3] Kukosa hewa ya kupumua kwa bahati mbaya kutokana na kutumia kitanda kimoja (pia hujulikana kama kulala pamoja) au vitu laini pia vinaweza kuchangia.[2][10] Sababu nyingine ya hatari ni kuzaliwa kabla ya wiki 39 za ujauzito.[7] SIDS husababisha takriban asilimia 80% ya vifo vya ghafla na visivyotarajiwa vya watoto wachanga (SUIDs).[2] Asilimia nyingine 20% ya visa mara nyingi husababishwa na maambukizo, matatizo ya kijeni na matatizo ya moyo.[2] Ingawa unyanyasaji wa watoto kwa njia ya kuwakosesha pumzi kimakusudi unaweza kuchunguzwa na kutambuliwa kimakosa kama SIDS, hili linaaminika kusababisha chini ya asilimia 5% ya visa.[2]
Njia bora zaidi ya kupunguza hatari ya SIDS ni kumlaza chali (kwa mgongo) mtoto mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja wakati wa kulala.[7] Hatua zingine ni pamoja na kutumia godoro dhabiti lililotenganishwa lakini lililo karibu na walezi, kutokuwepo matandiko yaliyolegea, mazingira ya kulala yenye ubaridi kiasi, kutumia titibandia na kuzuia kuwafidua kwenye moshi wa tumbaku.[5] Unyonyeshaji na utoaji chanjo pia vinaweza kuwa kinga.[5][6] Hatua ambazo hazijathibitishwa kuwa muhimu ni pamoja na vifaa vya kuhakikisha kuwa watoto wamelala sawasawa na skrini za kuwafuatilia watoto.[5][6] Ushahidi hautoshi kuhusiana na matumizi ya feni.[5] Huduma za kuziliwaza familia zilizoathiriwa na SIDS ni muhimu, kwani kifo cha mtoto mchanga hutokea kwa ghafla na bila mashahidi na mara nyingi huhusishwa na uchunguzi.[2]
Viwango vya SIDS hutofautiana karibia mara kumi katika nchi zilizoendelea kutoka mtoto moja kati ya watoto elfu moja hadi mtoto moja kati ya watoto elfu kumi.[2][11] Ulimwenguni kote, ugonjwa huu ulisababisha vifo vipatavyo 19,200 mwaka wa 2015, na idadi hii ikawa imeshuka chini kutoka kwa vifo 22,000 vilivyotokea mwaka wa 1990.[12][13] SIDS ilikuwa kisababishi kikuu cha tatu cha vifo kwa watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja nchini Marekani katika mwaka wa 2011.[14] Ugonjwa huu ndio kisababishi cha kawaida zaidi cha kifo kwa watoto wa umri wa kati ya mwezi mmoja na mwaka mmoja.[7] Takriban asilimia 90% ya visa hutokea kabla ya umri wa miezi sita, na mara nyingi zaidi kati ya miezi miwili na minne.[2][7] Vifo hivi hutokea zaidi kwa wavulana kuliko wasichana.[7] Viwango vyake vimepungua katika maeneo yenye "uhamasisho wa kulala salama" kwa hadi asilimia 80%.[11]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Sudden Infant Death Syndrome (SIDS): Overview". National Institute of Child Health and Human Development. 27 Juni 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 Kinney HC, Thach BT (Agosti 2009). "The sudden infant death syndrome". The New England Journal of Medicine. 361 (8): 795–805. doi:10.1056/NEJMra0803836. PMC 3268262. PMID 19692691.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "What causes SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 12 Aprili 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 "Centers for Disease Control and Prevention, Sudden Infant Death". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 18, 2013. Iliwekwa mnamo Machi 13, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Moon RY, Fu L (Julai 2012). "Sudden infant death syndrome: an update". Pediatrics in Review. 33 (7): 314–20. doi:10.1542/pir.33-7-314. PMID 22753789.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 6.2 "How can I reduce the risk of SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 22 Agosti 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 "How many infants die from SIDS or are at risk for SIDS?". National Institute of Child Health and Human Development. 19 Novemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Optiz, Enid Gilbert-Barness, Diane E. Spicer, Thora S. Steffensen; foreword by John M. (2013). Handbook of pediatric autopsy pathology (tol. la Second). New York, NY: Springer New York. uk. 654. ISBN 9781461467113. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2017.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Scheimberg, edited by Marta C. Cohen, Irene (2014). The Pediatric and perinatal autopsy manual. uk. 319. ISBN 9781107646070. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2017.
{{cite book}}
:|first=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ "Ways To Reduce the Risk of SIDS and Other Sleep-Related Causes of Infant Death". NICHD. 20 Januari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 2 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 11.0 11.1 Duncan, Jhodie R.; Byard, Roger W. (2018), Duncan, Jhodie R.; Byard, Roger W. (whr.), "Sudden Infant Death Syndrome: An Overview", SIDS Sudden Infant and Early Childhood Death: The Past, the Present and the Future, University of Adelaide Press, ISBN 9781925261677, PMID 30035964, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Julai 2020, iliwekwa mnamo 2019-08-01
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ GBD 2013 Mortality Causes of Death Collaborators (Januari 2015). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMC 4340604. PMID 25530442.
{{cite journal}}
:|last=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Wang, Haidong; Naghavi, Mohsen; Allen, Christine; Barber, Ryan M.; Bhutta, Zulfiqar A.; Carter, Austin; Casey, Daniel C.; Charlson, Fiona J.; Chen, Alan Zian (Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980-2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/s0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281.
{{cite journal}}
: Invalid|display-authors=29
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hoyert DL, Xu JQ (2012). "Deaths: Preliminary data for 2011" (PDF). National Vital Statistics Reports. 61 (6): 8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-02-02.